Kasi Sana! Tazama Mnyororo wa Uzalishaji Treni ya Mwendo Kasi wa Kilomita 350 kwa Saa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2023

Ukipanda treni ya mwendo kasi hapa China, kuna uwezekano mkubwa wa kupanda treni iliyoundwa na Kampuni ya Treni ya Changchun ya CRRC ya China. Kiwanda cha kampuni hiyo kiko eneo la Lyuyuan katika Mji wa Changchun, Mkoa wa Jilin nchini China.

Ikiwa ni chanzo cha uzalishaji wa China wa vyombo vya reli na treni za mwendo kasi, hivi sasa treni zinazozalishwa na kiwanda hicho cha Changchun cha CRRC zinachukua asilimia 40 ya treni zote za mwendo kasi nchini China. “Kwa mara ya kwanza tumetimiza kasi ya kilomita 350 kwa saa, na pia teknolojia ya treni kujiendesha chini ya uangalizi wa binadamu ya kiwango cha GoA2. Teknolojia hii inajaza pengo la kiufundi katika historia ya Dunia ya kkuendesha kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa,” amesema Dong Xueyan, mhandisi mwandamizi wa kiwanda cha Changchun cha CRRC.

Mwaka huu inatimia miaka 10 tangu pendekezo la kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” litolewe. Hadi hivi sasa, bidhaa za Kiwanda cha Changchun cha CRRC zimeuzwa kwa nchi na maeneo zaidi ya 20 zikiwemo Marekani, Australia, Brazil, Israel, na Saudi Arabia.

Tazama video hii ili kupata picha ya mnyororo wa uzalishaji wa treni yenye mwendo kasi wa kilomita 350 kwa saa kwenye Kiwanda cha Changchun cha Kampuni ya CRRC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha