Wang Yi aitaka Marekani kuchukua hatua madhubuti kurejesha uhusiano kati ya China na Marekani kwenye njia sahihi

(CRI Online) Julai 14, 2023

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Wang Yi amesema kwamba Marekani inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kuufanya uhusiano kati ya China na Marekani urudi kwenye njia sahihi.

Bw. Wang amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kando ya mikutano ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN), akisistiza kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano kupitia mawasiliano ya kina na ya wazi, wakati wa ziara ya Blinken nchini China mwezi uliopita.

Ametoa wito kwa Marekani kuwa na mtazamo wa busara na wa kivitendo na kushirikiana na China katika mwelekeo mmoja ili kuendeleza mashauriano juu ya kanuni elekezi za uhusiano wa China na Marekani, kupanua njia za mawasiliano ya kidiplomasia na kiusalama, kuboresha ufanisi wa mawasiliano, na kurahisisha mabadilishano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha