

Lugha Nyingine
Wang Yi asema China na Russia kwa pamoja zinahimiza Dunia yenye ncha nyingi, demokrasia zaidi katika mahusiano wa kimataifa
Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mamabo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) (Kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov mjini Jakarta, Indonesia, Julai 13, 2023. (Xinhua/Xu Qin)
JAKARTA - Mwanadiplomasia mwandamizi wa China Wang Yi amesema siku ya Alhamisi kwamba China na Russia kwa pamoja zitahimiza Dunia yenye ncha nyingi na uhusiano wa kimataifa wa kidemokrasia.
Wakati akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov kando ya mikutano mfululizo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN), Wang, ambaye ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mamabo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kutokana na mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kuonekana katika karne moja iliyopita, China na Russia kwa pamoja zinaungana mkono katika kulinda masilahi yao halali na kufuata njia ya kuishi kwa ujirani mwema na kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.
Amesema, pande hizo mbili zinapaswa kufuata makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu, na kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na uratibu.
Akieleza kuwa China na Russia ni washirika wa mazungumzo wa ASEAN, Wang amesema kuimarisha ushirikiano na nchi za ASEAN kunafaa kwa ajili ya kuleta mapatano ya kikanda kuhusu maendeleo, kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi, na kuongeza ustawi na utulivu wa kikanda.
“China iko tayari kushirikiana na Russia kuunga mkono nafasi kuu ya ASEAN, kuzuia uingiliaji kati wa nguvu za nje, kuunga mkono nchi za ASEAN katika kudumisha mwelekeo sahihi wa ushirikiano wa Asia Mashariki na kulinda amani na utulivu uliopatikana kwa bidii katika eneo hili,” Wang amesema.
Kwa upande wake Lavrov amesema Russia iko tayari kushirikiana na China kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuimarisha zaidi uratibu wa kimkakati na kuongeza ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Pande hizo mbili pia zilibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha uratibu na ushirikiano chini ya mifumo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Jumuiya ya BRICS.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma