China na ASEAN zasisitiza kujitolea kuendeleza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2023

Mkurugenzi wa Ofisi ya  Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi (wa tano kushoto) akihudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) huko Jakarta, Indonesia, Julai 13, 2023. (Xinhua/Xu Qin)

Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi (wa tano kushoto) akihudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) huko Jakarta, Indonesia, Julai 13, 2023. (Xinhua/Xu Qin)

JAKARTA - China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) zimeapa kuendeleza ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na ASEAN (10+1) uliofanyika Alhamisi hapa.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi amesema, China na ASEAN zimetekeleza kikamilifu nia na kanuni za “Mkataba wa Urafiki na Ushirikiano wa Asia Kusini-Mashariki” (TAC), kupanua ushirikiano wa kunufaishana katika sekta zote, na kufuata njia sahihi ya kuwa na ujirani mwema wa kudumu, na kupata maendeleo na ustawi kwa pamoja.

“Pande zote mbili zimefanya kazi pamoja katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kujenga pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja, huku kwa pamoja zikihimiza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda, na kuunganisha msingi wa amani na utulivu” amesema Wang kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa ASEAN, waangalizi wa ASEAN na Katibu Mkuu wa ASEAN.

Amesema China itajitolea kwa maendeleo yenye ubora wa juu na kutoa fursa mpya kwa nchi zote kupitia mtindo wa maendeleo ya kisasa ya China. “China iko tayari kuimarisha mshikamano na uratibu na ASEAN ili kuendeleza mchakato wa maendeleo ya kisasa katika Asia” amesema.

Pande mbalimbali za Jumuiya ya ASEAN zimeishukuru China kwa kuunga mkono nafasi kuu ya ASEAN na ujenzi wa jumuiya hiyo. Zimeishukuru China kwa kuchukua uongozi katika kueleza nia yake ya kutia saini makubaliano kuhusu “Mkataba wa kutokuwa na Silaha za Nyuklia katika Kanda ya Asia Kusini Mashariki”.

Kwenye mkutano huo, Wang alikutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Indonesia, Brunei, Singapore, Vietnam, Russia na Australia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha