

Lugha Nyingine
NATO inaendeshwa kutegemea Marekani: Gazeti la New York Times
Picha hii iliyopigwa Aprili 6, 2022 ikionyesha sanamu na bendera kwenye makao makuu ya Jumuiya ya NATO huko Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zheng Huansong)
NEW YORK - Jumuiya ya NATO kutoka mwanzo wa kuanzishwa kwake, haikuwahi kuhusika kimsingi na kujenga nguvu za kijeshi; badala yake, iliazimia kuifunga Ulaya Magharibi kwenye mradi mkubwa wa utaratibu wa Dunia unaoongozwa na Marekani, ambapo ulinzi wa Marekani ulitumika kama nyenzo ya kufaidika katika kupata makubaliano juu ya masuala mengine, kama vile biashara na sera ya fedha, imesema makala ya maoni iliyochapishwa na Gazeti la The New York Times (NYT) siku ya Jumanne.
"Katika nyanja ya ulinzi, jumuiya ya NATO haikuwa kama ilivyotangazwa," makala hiyo imesema. "Kwa miongo kadhaa, Marekani imekuwa mtoa huduma mkuu wa silaha, vifaa, vituo vya anga na mipango ya vita."
Kuhusu ununuzi wa silaha za ulinzi, vigezo vya uendeshji wa pamoja, na ukubwa kamili wa sekta ya kijeshi na viwanda ya Marekani na vizuizi vya urasimu vya Brussels, vinapendelea kampuni za Marekani kwa gharama ya washindani wao wa Ulaya. "Jumuiya hiyo, kwa kushangaza, inaonekana kudhoofisha uwezo wa washirika kujilinda," imeeleza makala hiyo.
"Hata hivyo kitendawili ni cha juujuu tu. Kwa hakika, NATO inafanya kazi kama ilivyobuniwa na wapangaji mipango wa Marekani baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na kuifanya Ulaya kutegemea nguvu ya Marekani ambayo inapunguza nafasi yake ya kufanya umamuzi wake," imesema.
Makala hiyo inasema, Jumuiya ya NATO kabisa haina mpango wa gharama kubwa wa hisani, NATO inalinda ushawishi wa Marekani barani Ulaya kwa bei nafuu. Michango ya Marekani kwa NATO na mipango mingine ya usaidizi wa usalama barani Ulaya inachukua sehemu ndogo ya bajeti ya kila mwaka ya Pentagon -- chini ya asilimia 6 kwa makadirio ya hivi majuzi.
"Nchini Ukraine, muundo uko wazi. Washington itatoa usalama wa kijeshi, na mashirika yake yatafaidika na bonanza la oda za silaha za Ulaya, wakati raia wa Ulaya watagharamia gharama ya ujenzi mpya baada ya vita -- jambo ambalo Ujerumani iko tayari kutimiza kuliko ujengaji wa jeshi lake," makala hiyo imeongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma