Rais Xi Jinping akutana na rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2023

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwenye Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Julai 17, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwenye Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Julai 17, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte siku ya Jumatatu kwenye Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai hapa Beijing.

Rais Xi amesema kuwa alipokuwa Rais wa Ufilipino, Duterte alifanya uamuzi wa kimkakati wa kuboresha uhusiano na China, akiwa na mtazamo wa kuwajibika kwa watu na historia. Na kwamba, Uhusiano kati ya China na Ufilipino uliweza kurejea kwenye njia sahihi na kustawi, ikiwa ni ishara ya mchango muhimu ambao Duterte alitoa katika mabadilishano ya kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema China na Ufilipino zote ni nchi zinazoendelea barani Asia, maendeleo ya nchi hizo mbili yanatokana na ujirani mwema na mazingira ya kipekee ya kirafiki na familia ya Asia ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

“China inashikilia sera ya diplomasia ya ujirani mwema inayojumuisha upendo, udhati, kunufaishana na ujumuishi, na daima imekuwa ikijitolea kujenga urafiki na ushirikiano na majirani zake” amesema Rais Xi.

Amesema, China siku zote inatilia maanani uhusiano kati ya China na Ufilipino na iko tayari kushirikiana na Ufilipino ili kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili yenye mwelekeo thabiti na ya muda mrefu. Pia ameeleza matumaini yake kuwa Duterte ataendelea kuwa na nafasi na jukumu muhimu katika ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

Huku akiishukuru China kwa uungaji mkono wake muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Ufilipino, Duterte amesema kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya Ufilipino na China kunatumikia maslahi ya nchi hizo mbili na kuendana na matakwa ya watu wengi wa Ufilipino. Ameahidi kuendelea kuchangia katika kuhimiza urafiki baina ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha