![](/img/FOREIGN/2021/05/313146/static/imgs/rmlogo.png)
![](/img/FOREIGN/2021/05/313146/static/imgs/tit0.png)
Lugha Nyingine
Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (Chengdu Universiade) yakaribisha timu ya kwanza kutoka nje ya nchi
![]() |
Kundi la kwanza la ujumbe wa Timu ya Brazil kwa ajili ya Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (Chengdu Universiade) likiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chengdu Tianfu huko Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China Julai 17, 2023. (Xinhua/Xu Bingjie) |
CHENGDU - Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (Chengdu Universiade) imekaribisha kundi la kwanza la ujumbe wa timu kutoka nje ya nchi wakati maafisa wa ujumbe wa Brazil walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chengdu Tianfu siku ya Jumatatu.
Maafisa saba kutoka ujumbe wa Timu ya Brazil waliwasili kwa ndege ET636 na kupita taratibu za forodha bila changamoto yoyote.
"Chengdu ni mji mkubwa na wenye ustawi kwa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani na tuna furaha sana kuja hapa na kushiriki katika michezo," Kelly wa ujumbe wa Brazil amesema baada ya kuwasili, na kuongeza "ujumbe wa Timu ya Brazil unawasili na wanamichezo 215, na tunashiriki katika michezo 11."
Alessandro, Naibu Mkuu wa ujumbe wa Brazil, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye uwanja wa ndege kuwa ni mara yake ya pili kuzuru Chengdu, baada ya hapo awali kuja kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Wajumbe mwezi Machi.
"Tunataka kuingia mapema katika Kijiji cha FISU kwa ajili ya maandalizi ya baadaye. Michezo itafanikiwa hapa Chengdu na ninatumai wanamichezo kutoka Brazil watafanya vyema," amesema Alessandro.
Idara ya Forodha ya Chengdu imeboresha njia sita za huduma ya haraka na kuongeza mashine nane za kuthibitisha hali ya karantini ya afya na madirisha mawili ya kuthibitisha mizigo ili kuhakikisha kuruhusu kwa haraka kwenye forodha kulikopangwa vizuri wakati wa Chengdu Universiade.
Kwa mujibu wa Chen Yang, Naibu Kamishna wa Forodha wa Uwanja wa Ndege wa Shuangliu chini ya Idara ya Forodha ya Chengdu, idara hiyo imeandaa mazoezi mawili kwa ajili ya kuwasili na kuondoka kwa wajumbe wa michezo huo, yanayohusu afya na karantini, uthibitishaji wa mizigo, usalama wa bidhaa maalum na hali nyingine 10.
Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (Chengdu Universiade) itafanyika Chengdu kuanzia Julai 28 hadi Agosti 8.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma