

Lugha Nyingine
WHO yataka kuchukuliwa kwa hatua haraka kukabiliana na vifo vinavyoongezeka kutokana na hali ya joto kali barani Ulaya
Watu wakijipoza joto kwenye chemchemi ya maji huko Frankfurt, Ujerumani, Julai 8, 2023. (Xinhua/ Zhang Fan)
COPENHAGEN – Wakati ambapo vifo vya watu 60,000 vilitokea Ulaya mwaka jana kutokana na hali ya joto kali, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Ulaya Hans Kluge amesisitiza "haja kubwa na ya dharura" ya kukabiliana na janga la tabianchi.
Idadi ya vifo vya watu kutokana na hali ya joto kali "inatazamiwa kuongezeka mwaka hadi mwaka," Kluge amesema Jumanne.
Mtalii akijipoza joto kwenye chemchemi ya maji huko Dubrovnik, Croatia, Juai 12, 2023. (Grgo Jelavic/PIXSELL kupitia Xinhua)
"Maeneo hatari" ya sasa yanajumuisha Ulaya ya kusini na mashariki, Kluge amesema, huku akiuhimiza umma "kuangalia ripoti za hali ya hewa mara kwa mara, kufuata mwongozo wa serikali husika za nchi, na kujijulisha kuhusu hatari za afya zinazohusiana na hali ya hewa kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika."
"Zaidi ya kuendana na hali mpya halisi ya majira haya ya joto, lazima tuangalie miaka na miongo ijayo," amesema.
"Kuna haja kubwa na ya haraka ya kuchukua hatua za kikanda na kimataifa ili kukabiliana na janga la tabianchi, ambalo linaleta tishio kwa uwepo wa binadamu."
Watu wakila aiskrimu huku kukiwa na wimbi la joto kali huko Roma, Italia, Julai 10, 2023. (Xinhua/Jin Mamengni)
Kwa suluhu ya muda mrefu, Kluge anaamini kwamba kupitishwa na kuanza kutumika kwa Azimio la Budapest, kutachukua hatua za dharura, za pande zote za kukabiliana na changamoto za kiafya zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira, n.k., katika Kanda ya Ulaya ya WHO mapema mwezi huu, itachukua safari ya muda mrefu ya kushughulikia "athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi kwa afya yetu na kwa mfumo wa afya ."
"Hatua kuhusu mabadiliko ya tabianchi haziwezi kutegemewa kwa serikali au chama fulani cha kisiasa; kwa kweli inahitaji kuwa suala lisiloegemea upande wowote kisiasa na linalopiganiwa na pande zote za wigo wa kisiasa," Kluge amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma