Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi akutana na Kissinger, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2023

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya  Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Henry Kissinger mjini Beijing, China, Julai 19, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Henry Kissinger mjini Beijing, China, Julai 19, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Wang Yi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amekutana na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Henry Kissinger mjini Beijing siku ya Jumatano.

Kwenye mazungumzo yao Wang, amesema kwamba Kissinger ametoa mchango wa kihistoria katika maendeleo ya uvunjaji wa barafu wa uhusiano kati ya China na Marekani na kubeba jukumu lisiloweza kubadilishwa katika kuimarisha maelewano kati ya nchi hizo mbili. "China inathamini urafiki wake na marafiki wa zamani."

Wang amesema China inadumisha kiwango cha juu cha mwendelezo wa sera yake kuhusu Marekani na inafuata kanuni elekezi za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wa kunufaishana.

"Kanuni hizi tatu ni za msingi na za muda mrefu, na ni njia ya kutendeana kwa usahihi kati ya China na Marekani zikiwa nchi mbili kubwa," ameongeza.

Maendeleo ya China yana nguvu kubwa ya ndani na mantiki ya kihistoria isiyoweza kuepukika, Wang amesema, huku akiongeza kuwa haiwezekani kujaribu kuibadilisha China, na hata haiwezekani kuizuia China.

Akifafanua msimamo wa China kuhusu suala la Taiwan, Wang amesisitiza kuwa sera ya kuwepo kwa China moja ndiyo msingi wa hali ya kawaida ya suala la Taiwan.

"Kama Marekani inatumai kwa dhati kuwepo kwa utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan, inapaswa kupinga kwa uwazi 'kujitenga kwa Taiwan' na kuweka mstari wazi na shughuli za kujitenga za makundi ya kutafuta 'Taiwan Kujitenga."

Kwa upande wake Kissinger amesema Marekani na China zote zina uwezo wa kuleta ushawishi kwa Dunia, na kulinda uhusiano tulivu kati ya nchi hizo mbili kunahusiana na amani na utulivu wa Dunia na ustawi wa binadamu.

Kissinger amesema, haijalishi ni ngumu kiasi gani, pande zote mbili zinapaswa kutendeana kwa usawa na kudumisha mawasiliano, na ameongeza kuwa haikubaliki kujaribu kutenganisha upande mwingine. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha