China yazitaka pande husika kutatua suala la Usafirishaji Nafaka kwenye Bahari Nyeusi kupitia mazungumzo

(CRI Online) Julai 21, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, siku ya Alhamisi kwamba China inazitaka pande husika kwenye suala la Mpango wa Usafirishaji Nafaka wa Bahari Nyeusi kufanya mazungumzo na majadiliano ili kutatua vizuri suala la usalama wa chakula wa kimataifa.

Bi. Mao amesisitiza kuwa, msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine siku zote ni wazi, na pia China itaendelea kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Awali, Russia iliyojitoa kwenye makubaliano hayo ya usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi, ilitangaza kuwa meli yoyote ya uchukuzi inayokwenda Ukraine kupitia bahari hiyo itachukuliwa kuwa na malengo ya kijeshi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha