Watu 9 wafariki katika ajali ya ndege nchini Sudan

(CRI Online) Julai 24, 2023

Jeshi la Sudan limesema watu tisa wamefariki katika ajali ya ndege ya abiria iliyotokea Jumapili kwenye uwanja wa ndege wa Bandari ya Sudan katika Jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, ajali hiyo ilitokea baada ya ndege hiyo kuanguka kutokana na hitilafu za kiufundi wakati inapaa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu tisa waliouawa ni pamoja na wanajeshi wanne, lakini msichana mmoja alinusurika kwenye ajali hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha