

Lugha Nyingine
Zaidi ya raia 13 wauawa na askari mashariki mwa DRC
(CRI Online) Julai 24, 2023
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) katika Jimbo la Ituri, Jules Ngongo, amesema, askari wa jeshi hilo amewaua watu 13 kuanzia Jumamosi hadi Jumapili kwenye kijiji cha Nyamamba mkoani humo.
Ngongo amesema, wengi waliouawa ni ndugu wa askari huyo, wakiwemo watoto kumi, na kuongeza kuwa, chanzo cha shambulio hilo ni mgogoro wa kifamilia.
Mamlaka za kijeshi zimeunda tume ya upelelezi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma