Wang Yi afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor

(CRI Online) Julai 25, 2023

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi, amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Bi. Naledi Pandor mjini Johannesburg.

Kweye mazungumzo hayo yaliyofanyika Jumatatu, Wang Yi amesema, mfumo wa ushirikiano wa Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) ni jukwaa muhimu zaidi kwa wawakilishi wa nchi za masoko yanayoibuka na nchi kubwa zinazoendelea ili kuimarisha majadiliano na ushirikiano, na pia ni njia muhimu zaidi kwa nchi za Kusini na Kusini kufanya mawasiliano ya kimkakati.

Amesema China inaiunga mkono Afrika Kusini ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa BRICS na mwenyeji wa mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS, kupokea maombi ya nchi husika kushiriki kwenye ushirikiano wa BRICS, kuhimiza maendeleo na kupaza zaidi sauti ya BRICS, kulinda haki na usawa wa kimataifa, kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi, na kuleta utulivu katika dunia ya sasa iliyo katika hali ya taharuki na sintofahamu.

Bi. Pandor amesema, Afrika Kusini iko tayari kuongeza mawasiliano na China na nchi nyingine za BRICS ili kufanikisha mkutano huo na kuhimiza ushirikiano wa BRICS kufika katika ngazi ya juu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha