Serikali ya Mkoa wa Heilongjiang, China yachunguza kikamilifu ajali ya kuanguka kwa paa la ukumbi wa michezo mjini Qiqihar

(CRI Online) Julai 25, 2023

Ofisi ya habari ya serikali ya Mji wa Qiqihar, katika Mkoa wa Heilongjiang nchini China imetoa ufafanuzi kuhusu ajali ya kuanguka kwa paa la ukumbi wa michezo katika Shule ya Sekondari Namba 34 katika mji huo.

Kwa mujibu wa Meya wa mji huo Bw. Shen Hongyu, watu 11 wamefariki katika ajali hiyo iliyotokea Jumapili, wakiwemo walimu na wanafunzi.

Serikali ya Mkoa wa Heilongjiang imeunda timu ya pamoja ya uchunguzi, ambayo itachunguza kwa kina kujua chanzo cha ajali hiyo, na kuwajibisha wahusika kwa mujibu wa sheria.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha