BRI yaonyesha ahadi za China za kushikilia ushirikiano na maendeleo ya pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2023
BRI yaonyesha ahadi za China za kushikilia ushirikiano na maendeleo ya pamoja
Mhandisi kutoka Shirika la Reli la China akifanya kazi na mfanyakazi wa Bangladesh kwenye Mradi wa Daraja Kiunganishi cha Reli la Padma huko Dhaka, Bangladesh, Mei 2, 2023. (Xinhua)

DHAKA – Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) linaonyesha ahadi za China katika kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na maendeleo ya pamoja, Nasim Mahmmud, Mkurugenzi Mtendaji wa Centre for East Asia Foundation (CEAF), taasisi ya kujitegemea ya utafiti isiyo ya kisiasa, amesema kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua.

Amesema, BRI, iliyopendekezwa na China Mwaka 2013, imeonyesha maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, ikiwakilisha juhudi kubwa za China katika kuhimiza mawasiliano, biashara na ushirikiano wa kiuchumi katika dunia nzima.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, pendekezo hilo limehimiza mabadilishano ya kitamaduni, kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya kikanda, na kuboresha utandawazi wa kikanda, ambayo yote yameongeza ustawi wa pamoja kati ya nchi zinazoshiriki.

"Hasa kampuni za China zimekuwa muhimu nchini Bangladesh, kuleta teknolojia ya kisasa, ujuzi, na uwekezaji katika maeneo tofauti," Nasim amesema.

Nasim, ambaye pia ni mhariri mkuu wa Jarida la Belt and Road, amesema miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na barabara, madaraja na mitambo ya kuzalisha umeme, imewezeshwa na uwepo wa China, ikiharakisha maendeleo ya kiuchumi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi wa Bangladesh.

Ripoti ya Wajibu wa Kijamii wa Kampuni za China nchini Bangladesh iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa, kuna miradi 27 ya China katika sekta za uzalishaji wa umeme na nishati, ambayo inahakikisha muundo wa nishati nchini Bangladesh unakuwa anuai, pamoja na barabara kuu 12, madaraja 21 na njia saba za reli zilizojengwa na kampuni za China nchini Bangladesh.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kampuni za China nchini Bangladesh zimetoa takriban ajira 550,000 katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia, na hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa ajira kwa wenyeji.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha