Gazeti la The Nation yasema "Utaratibu wa Dunia unaowekwa kwenye msingi wa kanuni " wa Marekani unahitaji kufikiriwa upya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2023

Askari wa Hifadhi ya Kitaifa aliyevalia barakoa akionekana pamoja na jengo la Bunge la Marekani, Capitol Hill likiwa limefunikwa na ukungu kwa nyuma, huku moshi kutoka kwenye moto wa nyika nchini Canada ukileta hewa inayoathiri afya ya watu katika Pwani ya Mashariki, huko Washington, D.C., Marekani, Juni 7, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

Askari wa Hifadhi ya Kitaifa aliyevalia barakoa akionekana pamoja na jengo la Bunge la Marekani, Capitol Hill likiwa limefunikwa na ukungu kwa nyuma, huku moshi kutoka kwenye moto wa nyika nchini Canada ukileta hewa inayoathiri afya ya watu katika Pwani ya Mashariki, huko Washington, D.C., Marekani, Juni 7, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

NEW YORK - Makala iliyochapishwa kwenye Gazeti la “The Nation” siku ya Jumatatu imesema, kutokana na mazingira ya siasa za kijiografia yaliyobadilika katika muongo mmoja uliopita, na ushawishi wa Marekani ukipungua duniani kote, Washington haiwezi kuendelea kujitetea kuwa uingiliaji kati wake wote au kuhusika katika migogoro ni kwa ajili ya kulinda "utaratibu wa Dunia unaowekwa kwenye kanuni".

"Washington lazima ikubali kwamba marafiki na washirika mara nyingi wataenda zao wenyewe ikiwa masilahi yao hayaendani na ya Marekani katika Dunia," makala hiyo imesema.

Makala hiyo imesema, kwa uhakika, motisha za kujitenga kutoka "kanuni" za Washington zimefanywa kuwa za juu zaidi kuliko hapo awali kwa utekelezwaji mpana wa vikwazo vya nje ya mipaka kama kanuni kuu ya ufundi wa serikali ya Marekani.

Asilimia 40 ya akiba ya mafuta duniani iko chini ya vikwazo vya Marekani, na hivyo kusababisha shinikizo kubwa kwa wazalishaji na wanunuzi wa mafuta kuhamia kwenye mauzo ya mafuta yasiyohitaji dola ya Marekani, imesema makala hiyo.

Mwaka 2001, dola ya Marekani ilichangia asilimia 73 ya hifadhi ya fedha duniani, na mwaka huu, ni asilimia 58, ikiwa ni punguzo la asilimia 15. "Matatizo hayaishii kwa kuondoa matumizi ya dola," imebainisha.

"Utaratibu wa Dunia unaowekwa kwenye msingi wa kanuni” uko katika hali ya kuanguka wenyewe isiyoweza kurekebishika, imesema. Kukubali ukweli huo wa mambo na kuongoza msukumo wa mpango mpya, jumuishi zaidi na wa kifikra zaidi, wa kisiasa na kiuchumi ni kazi ambayo Marekani inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kukumbatia, imesema makala hiyo.

Marekani "inapaswa kutetea ugawaji wa kweli wa mzigo wa ushirikiano wa pande nyingi" kupitia taasisi na makubaliano yaliyopo na mapya, na "inaweza kuacha 'upolisi' wa utaratibu wa Dunia kama inavyoona inafaa, na kuwa mshiriki muhimu katika kuzikutanisha nchi mbalimbali ili kutatua matatizo yanayosumbua zaidi ya binadamu, " imeongeza makala hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha