Rwanda yazindua utoaji chanjo dhidi ya polio kwa watoto chini ya miaka 7

(CRI Online) Julai 26, 2023

Wizara ya Afya ya Rwanda imesema nchi hiyo imezindua kampeni ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio kwa nchi nzima kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani.

Mkuu wa kitengo cha chanjo katika Kituo cha Matibabu cha Rwanda Bwana Hassan Sibomana, amesema wahudumu wa afya ya jamii watatoa chanjo ya matone iliyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Ameongeza kuwa kampeni hiyo ya chanjo itakayofanyika kwa siku tano inawalenga watoto milioni 2.7 walio na umri wa chini ya miaka 7.

Mara ya mwisho ugonjwa polio kugunduliwa nchini Rwanda ilikuwa ni miongo mitatu iliyopita. Hatua hizo za sasa zinakuja baada ya WHO kutangaza kuwa mamlaka za afya nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimegundua maambukizi ya virusi hivyo katika nchi zao.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha