

Lugha Nyingine
Wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kichina miongoni mwa watoto wenye umri wa kwenda shule nchini Kenya waongezeka na kufikia 300
(CRI Online) Julai 26, 2023
![]() |
(Picha inatoka CRI.) |
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Mitaala ya Masomo nchini Kenya, Charles Ong’ondo amesema, idadi ya wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kichina miongoni mwa watoto wenye umri wa kwenda shule nchini Kenya imeongezeka na kufikia 300, wakati uhusiano kati ya China na Kenya ukiongezeka.
Bw. Ong’ondo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kando ya Mkutano wa Shirikisho la Mitaala ya Masomo la Afrika kuwa, lugha ya Kichina imeendelea kupata umaarufu tangu ilipoingizwa kwenye mtaala wa masomo miaka mitatu iliyopita.
Amesema Wizara ya Elimu nchini Kenya inatoa mafunzo kwa walimu Zaidi ili wanafunzi waweze kufundishwa lugha na utamaduni wa Kichina.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma