

Lugha Nyingine
Bibi Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Indonesia
(CRI Online) Julai 28, 2023
Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan jana Alhamisi alikutana na Mke wa Rais wa Indonesia Bibi Iriana Joko Widodo huko Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China.
Bibi Iriana anaambatana na Rais Joko Widodo ambaye atahudhuria hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu na kufanya ziara rasmi China.
Bibi Peng Liyuan na Bibi Iriana walitazama kazi za mikono za urithi wa utamaduni usioshikika na maonyesho ya sanaa ya chai.
Bibi Peng amesema China na Indonesia zinafurahia mshikamano wa kitamaduni na uhusiano wa karibu kati ya watu wa nchi hizo mbili, huku akitarajia kuwa pande hizo mbili zitazidisha urafiki kati yao.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma