Lugha Nyingine
Siku ya pili ya Michezo ya Vyuo Vikuu ya Dunia ya Chengdu: China yaongoza kwa kuwa na medali tisa za dhahabu
CHENGDU, Julai 30 (Xinhua)
Timu ya China inaendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia FISU inayoendelea mjini Chengdu, Mkoani Sichuan, na kuongoza kwa idadi ya medali ikiwa na medali tisa za dhahabu. Kinyang’anyiro cha kusaka medali ya dhahabu kiliendelea kwenye mchezo wa Wushu, ambapo jana Jumapili China ilipata medali tatu za dhahabu, baada ya kupata medali nne za dhahabu katika siku iliyotangulia.
Mchezaji wa China Cao Maoyuan alipata ushindi katika mchezo wa Nangun kwa wanaume.
Baada ya kunyakua dhahabu ya kwanza kwenye mchezo wa Nanquan kwa upande wa wanaume, mchezaji wa China Cao Maoyuan alishinda mara mbili, jana pia alipata ushindi katika mchezo wa Nangun kwa wanaume. Cao ameeleza nia yake ya kuendelea kufanya juhudi ili kupata ushindi zaidi katika mchezo wa wushu.
Mchezaji mwingine wa China Jin Zhedian pia alipata medali yake ya pili ya dhahabu yake kwenye mchezo wa Daoshu kwa wanaume, na kusisitiza kuwa ataendelea kujifunza zaidi kutoka kwa wachezaji wageni.
Mchezaji wa China Chen Xiaoli alipata ushindi katika mchezo wa Taijijian.
Kwa upande wa wanawake mchezaji wa China Chen Xiaoli alipata ushindi katika mchezo wa Taijijian.
Katika mchezo wa kurusha mishale, China ilijiweka sawa na kumshinda bingwa mtetezi wa Korea Kusini kwa seti 5-4 na kuwania taji la timu ya wanawake. Mchezaji wa Korea Kusini Lee Ga-hyun alipata mishale miwili katika jaribio la kwanza, na kuifanya China kuongoza kirahisi . Hata hivyo, Korea Kusini walipata nguvu katika seti mbili zilizofuata, wakijipatia alama 55 mbili zaidi dhidi ya 53 za timu ya China, wakiongoza kwa seti 4-2. Timu ya China haikukata tamaa, ilishinda seti ya nne kwa alama 54-53 na kufanya iwe sare ya seti 4-4, na kufanya msingi apatikana kwenye raundi ya mwisho. Katika raundi ya mwisho, Korea Kusini ilipata seti 8, huku China ikipata seti 9, na kuendelea kuongoza kwa ushindi huo mdogo hadi mwisho mwa mchezo.
Mapema kabla ya japo timu ya wanaume ya China ilipata ushindi katika mchezo wa jumla. Walenga shabaha walipata ushindi katika siku ya pili ya shindano hilo, na kuongeza dhahabu mbili zaidi kwenye hesabu ya medali za China.
Kwenye mchezo wa rhythmic gymnastics, China ilifanya vizuri na kupata medali ya dhahabu kwa ushindi wa pointi 57.150. Nahodha wa timu hiyo Xiao Mingxin, amesema kwenye mchezo wao wameunganisha Kung Fu kwenye mchezo wa miduara mitano na kuingiza wimbo wa watu wa Sichuan kwenye mchezo wa tepe tatu na mipira miwili, ambayo iliwasaidia kufanya vizuri sana.
Na kwenye mchezo wa taekwondo, timu ya China imenyakua medali ya dhahabu katika mchezo wa mchanganyiko.
Kwa sasa China inaongoza kwa kuwa na medali 13 za dhahabu, nne za fedha na tatu za shaba, ikifuatiwa na Japan na Korea Kusini kwa medali tisa na nane mtawalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma