China yaendelea kukabiliana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2023

Wafanyakazi wa usafi wakisafisha barabara katika eneo la Mentougou mjini Beijing lililokumbwa na mafuriko. Julai 31, 2023. (Xinhua/Ju Huanzong)

Wafanyakazi wa usafi wakisafisha barabara katika eneo la Mentougou mjini Beijing lililokumbwa na mafuriko. Julai 31, 2023. (Xinhua/Ju Huanzong)

Serikali ya China imeanza juhudi kubwa za uokoaji na kutoa misaada katika kukabiliana na mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga, ambayo hadi sasa imesababisha vifo vya watu 11 katika mji wa Beijing.

Mvua zilizoendelea kunyesha tangu Jumamosi usiku zimeathiri zaidi ya watu 44,600 katika maeneo 13 ya Beijing, na kusababisha watu 127,000 kuhamishiwa mahali pengine.

Mvua kubwa iliyosababishwa na Kimbunga cha Doksuri, imenyesha katika eneo kubwa la kaskazini mwa China na maeneo kando ya mto Manjano na Mto Huaihe. Mvua hiyo imesababisha mafuriko na madhara ya kijiolojia, na kusababisha hasara kubwa katika mji wa Beijing na mkoa wa Hebei.

Rais Xi Jinping wa China jana alipokuwa anatoa maelekezo ya kazi kuhusu kuzuia mafuriko na kutoa msaada kwa wahanga wa mafuriko, alitoa wito wa kuwatafuta na kuwaokoa watu wote ambao hawajulikani walipo, au wale waliokwama kwenye mafuriko.

Wizara ya Rasilimali za Maji ya China imedumisha mwitikio wa dharura wa ngazi ya pili kwenye eneo la Beijing-Tianjin-Hebei kaskazini mwa China, na kutuma timu 10 za kukabiliana na mafuriko katika eneo hilo na mikoa mingine.

Picha hii iliyopigwa tarehe 31 Julai 2023 inaonyesha maji yakitiririka kutoka kwenye Bwawa la Huangbizhuang huko Luquan, Shijiazhuang Mkoani Hebei kaskazini mwa China. (Picha na Bai Yunfei/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa tarehe 31 Julai 2023 inaonyesha maji yakitiririka kutoka kwenye Bwawa la Huangbizhuang huko Luquan, Shijiazhuang Mkoani Hebei kaskazini mwa China. (Picha na Bai Yunfei/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha