Michezo ya vyuo vikuu ya dunia ya Chengdu | China yaishinda Japan na kupata ubingwa mpira wa wavu kwa wanawake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2023

Gao Yi wa China (Namba 6) na Wu Mengjie (Namba 5) wakiruka ili kuzuia mpira wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa wavu kwa wanawake dhidi ya Japan kwenye michezo ya vyuo vikuu ya dunia inayoendelea huko Chengdu, Agosti 6, 2023. (Xinhua/Cao Yiming)

Gao Yi wa China (Namba 6) na Wu Mengjie (Namba 5) wakiruka ili kuzuia mpira wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa wavu kwa wanawake dhidi ya Japan kwenye michezo ya vyuo vikuu ya dunia inayoendelea huko Chengdu, Agosti 6, 2023. (Xinhua/Cao Yiming)

Timu ya China imeishinda Japan kwa seti mfululizo na kutwaa medali ya dhahabu kwenye mchezo wa mpira wa wavu kwa wanawake uliofanyika jumapili, kwenye michezo ya vyuo vikuu ya dunia inayoendelea huko Chengdu.

CHENGDU, Agosti 6 (Xinhua)

China imeishinda Japan kwa seti 29-27, 29-27, 25-22 na kutwaa medali ya dhahabu kwenye mchezo wa mpira wa wavu kwa wanawake uliofanyika Jumapili, kwenye michezo ya vyuo vikuu ya dunia inayoendelea huko Chengdu.

China iliwahi kuongoza kwa pointi tano katika dakika za mwanzo za mchezo, lakini baadaye Japan iliongeza kasi. Baada ya Japan kuokoa pointi tano, Wang Wenhan alipata pointi ya ushindi na kuisaidia China kupata chukua seti ya kwanza.

Seti ya pili ilikuwa na upinzani mkali, na Japan ilikuwa ya kwanza kupata pointi, lakini ilikuwa ni China ambayo hatimaye ilishinda kwa seti 2-0.

Timu ya China ilifanikiwa kulinda uongozi wake katika seti ya tatu. Zhong Hui alifanikiwa kupata point na kuipatia China ubingwa kabla ya Japan kufanya makosa kwenye kupiga mpira.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha