Mgogoro wa Ethiopia wasababisha watu 12,000 kukimbia makazi yao

(CRI Online) Agosti 07, 2023

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA) hivi karibuni imesema, mgogoro kwenye mkoa wa Gambella, Magharibi mwa Ethiopia umesababisha watu zaidi ya 12,000 kukimbia makazi yao.

Katika ripoti yake kuhusu hali ya Ethiopia, UNOCHA imesema, watu hao wamekimbia makazi yao kutokana na mgogoro wa kimabavu uliotokea hivi karibuni mkoani Gambella, na wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Ripoti hiyo imesema watu hao wanahitaji makazi ya dharura na msaada usio wa chakula, ambao ni pamoja na vifaa vya lishe kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, na vifaa muhimu kwa wanawake na wasichana.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha