

Lugha Nyingine
Rais wa Nigeria azindua mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme unaojengwa na kampuni ya China
(CRI Online) Agosti 07, 2023
Rais wa Nigeria Bola Tinubu amezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme wa gesi unaofanywa na kampuni ya Uhandisi wa Mashine ya China.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, rais Tinubu amesema mradi huo ni muhimu sana kwa Nigeria, na pia ni hatua ya kwanza katika juhudi za serikali za kuanzisha sekta yenye nguvu ya nishati ambayo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Naye Balozi wa China nchini Nigeria, Cui Jianchun, ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua, kuwa mradi huo utachukua nafasi muhimu katika kuisaidia Nigeria kuondoa pengo la upatikanaji wa umeme. Ameongeza kuwa, utakapokamilika, mradi huo unatarajiwa kukabiliana na mahitaji ya umeme kwa mji mkuu wa Nigeria na maeneo ya jirani.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma