Watu 17 wauawa kwenye mashambulizi mawili katikati mwa Mali

(CRI Online) Agosti 08, 2023

Mamlaka ya mkoa wa Bandiagara nchini Mali jana imetoa taarifa ikisema, watu 17 wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Shambulizi la kwanza lilitokea Jumamosi kwenye kijiji cha Bodio, na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine wawili kujeruhiwa, na watu wengine wawili waliuawa kwenye shambulizi lingine lililotokea Jumapili kwenye mgodi ulioko kati ya kijiji cha Bodio na kijiji cha Anakanda.

Mashambulizi hayo yalitokea siku moja baada ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali kukabidhi kambi ya Ogossagou huko Bandiagara, kwa serikali ya Mali.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha