Watu 11 wafariki na wengine 40 hawajulikani walipo kufuatia ajali ya boti nchini Tunisia

(CRI Online) Agosti 08, 2023

Msemaji wa Mahakama ya Mwanzo ya Sfax, Tunisia Bw. Faouzi Masmoudi amesema watu 11 wamefariki na wengine zaidi ya 40 hawajulikani walipo baada ya boti moja kuzama katika bahari karibu na mkoa wa Sfax mashariki mwa Tunisia hapo jana.

Msemaji huyo amesema boti hiyo ilibeba wahamiaji haramu 57, wengi wao kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara. Walinzi wa pwani ya Tunisia waliokoa miili 11 kwenye bahari karibu na kisiwa cha Kerkennah katika mkoa wa Sfax na kuokoa watu wawili, na bado wanaendelea kuwatafuta wengine waliozama baharini.

Habari zinasema, boti hiyo iliondoka kutoka Jimbo la Sfax siku chache zilizopita kuelekea nchini Italia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha