Afrika Kusini iko tayari kuandaa mkutano wa BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2023

Picha iliyopigwa Machi 7, 2023 ikionyesha mawio ya jua mjini Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha imepigwa na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

Picha iliyopigwa Machi 7, 2023 ikionyesha mawio ya jua mjini Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha imepigwa na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor, amesema Afrika Kusini iko tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa 15 wa nchi za BRICS unaosubiriwa na wengi.

JOHANNESBURG, Agosti 8 (Xinhua)

Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor, amesema Afrika Kusini iko tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa 15 wa nchi za BRICS unaosubiriwa na wengi.

Akiongea na wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofanywa na Afrika Kusini kuhusu mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kati ya Agosti 22 na 24, Bibi Pandor amesema, "Rais Ramaphosa amethibitisha utayari wa Afrika Kusini kuandaa mkutano wa 15 wa ana kwa ana wa kundi la BRICS, huko Sandton, Johannesburg. Kwa hiyo rais amewaalika viongozi 67 kutoka nchi za Afrika na Kusini mwa dunia kuhudhuria mazungumzo ya BRICS-Afrika na mazungumzo ya BRICS Plus."

Wang Yi (kulia), mkurugenzi wa Ofisi ya  Kamati ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akutana na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 24, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong )

Wang Yi (kushoto), mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akutana na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 24, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong)

Bibi Pandor amesema viongozi walioalikwa kuhudhuria mkutano huo wanawakilisha mabara yote na maeneo yote za nchi za kusini mwa dunia.

Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa mkutano huo chini ya kaulimbiu "BRICS na Afrika: Ushirikiano wa ukuaji unaoharakishwa kwa Pamoja, Maendeleo Endelevu, na Ushirikiano wa Kimataifa."

Bibi Pandor pia amesema wakati wa mkutano huo, Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa kongamano la biashara la nchi za BRICS, Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS, pamoja na kuendesha mikutano mingine.

Amefafanua kuwa viongozi wa BRICS wanatarajiwa kujadili fursa za kutambua uwezo kamili wa BRICS wa kufufua uchumi wa dunia nzima na maendeleo endelevu.

BRICS ni kifupi cha nchi tano zinazoibukia kiuchumi -- Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Afrika Kusini ilipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kundi hilo Januari 1, 2023, ikichukua nafasi hiyo kutoka kwa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha