Rose kutoka Uganda aliyeoana na mwanamume wa Zhejiang, China awa TikToker maarufu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2023

Hivi karibuni, Tiktoker maarufu Rose aliyetoka Uganda na kuishi mkoani Zhejiang, nchini China amerudi nyumbani kwake pamoja na mumewe na mwanawe, na safari yao imepata ufuatiliaji mkubwa kutoka watu wa China na nchi nyingine mbalimbali mtandaoni. Televisheni ya mkoa wa Zhejiang wa China, televisheni ya kitaifa ya Uganda na vyombo vingine vya habari vimetoa ripoti kuhusu safari hiyo.

Katika video zilizochapishwa na Rose kwenye akaunti yake, alikumbatana na wazazi wake na ndugu zake kwa msisimuko, na mumewe aliwapa zawadi walizoleta kutoka China. Pia waliwanunulia vyombo vya umeme nyumbani katika maduka ya wachina huko Uganda, na hata walinunua kondoo mmoja kama zawadi.

Watu wengi walionesha ufuatiliaji wao na matumaini yao kwa safari ya Rose ya kurudi nyumbani. Kwenye ukurasa wake wa Facebook, kuna Wauganda walioandika kuwa wanawakaribisha Rose na wenzake.

Rose na mama yake walikuwapo kwenye hospitali huko Uganda. Chanzo:

Rose alileta mama yake kwenye hospitali kwa ajili ya kupimwa afya na madaktari wa China wanaotoa msaada wa matibabu nchini Uganda. Chanzo: Shirika la Televisheni ya Zhejiang

Kuanzia mwaka 2021, Rose ameanza kuchapisha video kwenye Douyin (TikTok wa China) na Xiaohongshu, ambazo zote ni majukwaa makuu ya mitandao ya kijamii ya China. Hadi sasa idadi ya wafuasi wake imezidi milioni kumi, akiwa mmoja wa watengenezaji video wenye wafuasi wengi zaidi kutoka nchi za nje kwenye majukwaa hao wawili. Baadaye Rose alichapisha video zake kwenye mitandao ya kijamii ya kimataifa, ikiwemo TikTok, Youtube na Facebook n.k..

Rose aliyezaliwa mwaka 1993 aliishi kijijini mwa Uganda. Miaka 8 iliyopita, alifahamiana na rafiki mmoja kutoka China alipofanya kazi huko Kampala, ambaye ni dada mdogo wa mwanamume atakayekuwa mume wake siku za mbele, Wu Jianyun. Baada ya kufahamishwa na rafiki huyo kwa Wu, Rose alianza kupendana naye akaamua kuonana na kuhama nchini China ili kuishi pamoja naye. Rose na Wu walioana katika Mji wa Lishui wa Mkoa wa Zhejiang wa China mwezi wa Aprili, 2015. Kwa sababu ya sifa zake za kuwa na hekima na kufanya kazi kwa bidii, Rose alisikilizana na wenyeji kwa haraka.

Video za Rose zinakumbuka maisha yake ya kila siku. Kwenye video hizi, Rose anaongea vizuri lugha ya Kichina, kupika chakula cha Kichina, na hata kuonesha mchakato mzima wa kupika chakula kutoka shambani hadi mezani. Rose pia ameonesha kipaji chake cha kuzungumzana na majirani na wanafamilia kwa kutumia lugha ya Kichina. Inafahamika kuwa stadi zake za kupika amezijifunza kutoka kwa mumewe na shemeji zake.

Rose na mumewe na mwanawe wakila chakula pamoja. Picha ilichukuliwa kutoka video ya Rose.

Rose na mumewe na mwanawe wakila chakula pamoja. Picha ilichukuliwa kutoka video ya Rose.

Video za Rose zinapendwa sana na Wachina bali pia watu wa nchi nyingine mbalimbali, hata Wachina wengi wamesema wanataka kujifunza kupika chakula cha Kichina kutoka kwa Rose. Chini ya video yake kuna mtu aliyeandika maoni kuwa, “Kutazama video zake ni kama kutazama tamthilia za televisheni kuhusu maisha ya kijijini zinazotuliza moyo wangu.”

Hivi sasa Rose ana timu ya kutengeneza video yenye wafanyakazi watano, na wanatengeneza video fupi kwenye Kijiji Ye, nyumbani kwa mumewe Wu. Ndani ya mwezi wa kwanza wa mwaka 2023, idadi ya wafuasi wa akaunti yake ya Youtube imeongezeka kutoka 12,000 hadi 136,000, na hivi sasa ana wafuasi 298,000. Akaunti yake ya TikTok ina wafuasi milioni 1.2, ikiwa ni akaunti yenye wafuasi wengi zaidi ya Uganda.

Akaunti ya TikTok ya Rose.

Akaunti ya TikTok ya Rose.

Mwezi wa Juni, mwaka huu, serikali ya Lishui ilipongeza watengenezaji video za kutangaza vyakula huko na maisha huko waliofanya vizuri zaidi, ambapo Rose pia alitambulishwa na serikali hiyo kwa watu wote wa China. Katika miaka ya hivi karibuni, China imetoa sera ya kustawisha vijiji, na serikali ya mji wa Lishui pia imeendeleza kwa hamu utalii na sekta nyingine vijijini, ili kuwasaidia wakulima kuboresha maisha yao. Rose alisema, alipokwenda kwenye Lishui, kulikuwa na nyasi tu mbele nyumba yao, lakini sasa kuna barabara ya saruji. Wakazi wengi wa kijiji hicho wanaishi kwenye nyumba zilizojengwa upya.

Rose anafurahia sana maisha yake ya sasa, na ana matumaini kuhusu siku za mbele. Alisema, “wanafamilia tunaishi pamoja, mtoto anakua kwa afya njema na furaha, hii kwangu maisha bora.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha