Watu sita wauawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa kando ya barabara nchini Somalia

(CRI Online) Agosti 10, 2023

Gavana wa mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia Bw. Mohamed Ibrahim Barre jana amethibitisha kuwa, abiria sita wakiwemo watoto watatu wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria walilokuwa wakisafiria kukanyaga kifaa cha mlipuko mkoani humo.

Bw. Barre amesema basi hilo lilikuwa linatokea mji wa Marka kuelekea mji wa Qoryoley, na anaamani kuwa shambulio hilo limefanywa na kundi la al-Shabaab.

Bado hakuna kundi lolote linalotangaza kuwajibika na tukio hilo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha