

Lugha Nyingine
Zaidi ya watu 20 wauawa kwenye mashambulizi dhidi ya vijiji viwili katikati mwa Nigeria
(CRI Online) Agosti 11, 2023
Vyombo vya habari nchini Nigeria jana vimesema, watu zaidi ya 20 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha dhidi ya vijiji viwili kwenye jimbo la Plateau, katikati mwa nchi hiyo lililotokea jumatano wiki hii.
Vikosi vya Nigeria katika jimbo la Plateau jana vilitoa taarifa ikisema, watu hao hawakushambulia kituo cha ukaguzi cha jeshi hilo, na badala yake kushambulia vijiji hivyo.
Vikosi vilivyokuwa kwenye eneo hilo vilifika haraka kwenye eneo la tukio na kujibu mashambulizi.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma