

Lugha Nyingine
Reli iliyojengwa na China yaleta neema mpya kwa Wakenya
Madereva wa treni nchini Kenya wakijifunza taratibu za uendeshaji wa treni kutoka kwa mwalimu wao Mchina wakati wa mafunzo mjini Nairobi, kabla ya kuanza kwa treni ya SGR kati ya Mombasa-Nairobi. SUN RUIBO/XINHUA
NAIROBI — Msimamizi wa idara ya Reli ya Kisasa ya Mombasa-Nairobi (SGR) iliyojengwa na China, Bw. Lawrence Pius Murithi anajivunia kupata ajira nzuri ambayo wenzake wengi wameshindwa kuipata. Kabla ya reli hiyo yenye urefu wa kilomita 480 kuanza kazi Mei 31, 2017, kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 alinufaika kutokana na mafunzo kuhusu matengenezo ya treni za abiria, yaliyofadhiliwa na mkandarasi wa reli ya SGR.
Bwana Murithi amesema alikuwa na bahati kujiunga na kampuni ya ujenzi wa reli ya SGR katika sehemu ya matengenezo ya treni za abiria, na kufurahia umahiri wa wakufunzi wake wachina kwenye kazi yao.
Katika kipindi cha miaka sita iliyopita tangu ajiunge na timu ya wafanyakazi inayokua ya vijana wa Kenya wanaofanya kazi kwenye reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi, Bwana Murithi ameongeza ujuzi wake wa kiufundi, wa usimamizi na hata binafsi. Pia amesema ameboresha hali yake ya kifedha, kutokana na mshahara mzuri anaopata kila mwezi ambao umemwezesha kununua ardhi katika kijiji chao na kuendesha biashara ya mifugo kama chanzo cha ziada cha mapato.
Akikumbuka hali ya zamani, Bwana Murithi alionyesha kuwa na uchungu akieleza jinsi ambavyo maisha yake yangekuwa bila kuwa na usalama wa kifedha, akionyesha usalama wa kifedha alioupata kutokana na kufanya kazi kwenye reli hiyo, akiahidi kuwashauri vijana wenzake kuwa na ndoto za kufanya kazi ya kifahari kama yeye.
Tangu reli ya SGR ianze kufanya kazi miaka sita iliyopita, reli hiyo imeharakisha kuboresha maisha ya wafanyakazi wake, ikiajiri kundi la wataalamu vijana kufanya kazi katika sehemu muhimu kama vile vichwa vya treni, njia ya reli, njia za mawasiliano na hata usimamizi.
Reli hiyo inayosifiwa kwa kuleta mapinduzi ya usafiri na biashara kwenye eneo la Afrika Mashariki ikiwa na urefu wa kilomita 480, imechangia ukuaji wa pato la taifa la Kenya kwa asilimia 1.5. Reli hiyo ni mradi mkuu wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” la China ambalo limesaidia kuleta ujuzi na uhamishaji wa teknolojia, na kuwanufaisha vijana wa Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma