

Lugha Nyingine
China yaendelea na juhudi za kukabiliana na mafuriko na vimbunga
Wazima moto wakiwa wanasafisha barabara iliyochafuliwa na mafuriko katika mji wa Shangzhi, kaskazini-mashariki mwa Mkoa wa Heilongjiang China, Agosti 11, 2023. (Xinhua/Zhang Tao)
BEIJING, Agosti 13 (Xinhua)
Mamlaka za China zimefanya mkutano kwa njia ya video kujadili hali ya mvua, maji na maafa ya kijiolojia, pamoja na athari zinazoweza kusababishwa na vimbunga. Mkutano huo uliweka mipango ya kujilinda dhidi ya mafuriko na vimbunga, hasa katika maeneo muhimu ya Tianjin, Liaoning, Chongqing na Shaanxi.
Kuanzia Jumapili hadi Jumatatu mvua kubwa itanyesha tena katika maeneo ya kaskazini-mashariki, kaskazini-magharibi na kusini-magharibi mwa China, huku maeneo mengine yakitazamiwa kuwa na hali mbaya ya hewa. Mkutano huo umehimiza mikoa hiyo kuimarisha ufuatiliaji, vikosi vya ulinzi na uokoaji wa dharura, kuchunguza kisayansi na kuondoa hatari, na kuharakisha kazi za urejeshaji wa kingo za maji.
China imedumisha mwitikio wa dharura wa ngazi ya pili kwa mafuriko mjini Tianjin, ngazi ya tatu kwa mji wa Beijing, na mikoa ya Hebei, Heilongjiang na Jilin, na ngazi ya nne kwa mafuriko na kimbunga huko Liaoning. Timu za kazi zilizotumwa katika hatua za awali zitaendelea kusaidia kazi zinazofanywa na maeneo ya makazi kuzuia mafuriko na kukabiliana na kimbunga katika maeneo yaliyotajwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma