Rais Xi Jinping atoa maagizo katika Siku ya Kwanza ya Taifa ya Ikolojia ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2023

HANGZHOU - Rais wa China Xi Jinping ameitaka jamii nzima kuhimiza kwa dhati na kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza dhana kwamba maji safi na milima yenye uoto uliostawi ni mali ya thamani kubwa.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa maagizo hayo katika Siku ya Kwanza ya Kitaifa ya Ikolojia ya China Agosti 15.

“Uhifadhi wa ikolojia ni muhimu sana kwa maendeleo endelevu ya Taifa la China,” Rais Xi amesema, huku akilitaja kuwa suala kuu la kisiasa ambalo linahusu dhamira na madhumuni ya CPC pamoja na suala kuu la kijamii ambalo linahusu ustawi wa umma.

Amesema, katika safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote, juhudi zinapaswa kufanywa ili kudumisha azma ya kimkakati katika kuendeleza maendeleo ya kiikolojia na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu yanayotilia maanani ulinzi wa kiwango cha juu wa mazingira.

Ameeleza kwamba, kwa kujikita katika kufikia kilele cha utoaji wa kaboni na kusawazisha utoaji wa kaboni, China inapaswa kuwezesha kuhama kwa utaratibu kutoka kwenye udhibiti wa pande mbili juu ya kiasi na ukubwa wa matumizi ya nishati hadi udhibiti wa pande mbili juu ya kiasi na ukubwa wa utoaji wa kaboni.

“Jitihada zinapaswa kufanywa kuhimiza kuhama kuelekea mbinu na mtindo wa maisha na uzalishashaji wenye kutumia nishati safi na kutoa kaboni chache, na kuharakisha maendeleo ya kisasa katika hali ya mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili ili kujenga China Nzuri katika mambo yote,” Rais Xi amesema.

Rais Xi ametoa wito wa kufanya juhudi kwa hiari na za mara kwa mara katika jamii ili kutoa mchango mkubwa kwa pamoja kujenga Dunia safi na nzuri.

Maagizo hayo ya Rais Xi yametolewa na Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang kwenye hafla ya shughuli ya Siku ya Kwanza ya Taifa ya Ikolojia ya China iliyofanyika Jumanne katika Mji wa Huzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China.

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akizungumza kwenye hafla ya  kuanzishwa kwa shughuli ya Siku ya Taifa ya Ikolojia ya China katika Mji wa Huzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. Agosti 15, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

Shughuli ya Siku ya Taifa ya Ikolojia ya China ikifanyika katika Mji wa Huzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Agosti 15, 2023. (Xinhua/Jiang Han)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha