Marekani bado inatilia mkazo suluhu ya kidiplomasia juu ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Niger: Blinken

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2023
Marekani bado inatilia mkazo suluhu ya kidiplomasia juu ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Niger: Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Uhusiano wa Kigeni ya Seneti ya Marekani kwenye Bunge la Marekani, Capitol Hill mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 26, 2022. (Picha na Ting Shen/Xinhua)

WASHINGTON - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Jumanne kwamba Marekani bado "inatilia mkazo sana diplomasia" kama chombo cha kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Niger unaotokana na jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

"Tunaendelea kutilia mkazo sana njia ya diplomasia kwa ajili ya kufikia matokeo tunayotaka, ambayo ni kurejea kwa utaratibu wa katiba," Blinken amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, na kuongeza kuwa anaamini kuwa bado kuna nafasi ya kutimiza lengo hilo kwa njia ya diplomasia.

Kauli ya Blinken inakuja wakati mvutano ukiendelea kuzuka ndani na jirani na nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilitangaza siku ya Alhamisi kuanzishwa na kutumwa kwa "kikosi cha utayari kwa ajili ya kurejesha utaratibu wa katiba" nchini Niger.

Uamuzi huo umetolewa na marais na maafisa wakuu wa nchi wanachama wa ECOWAS, walipokuwa wakihitimisha mkutano wa kilele mjini Abuja, Nigeria, unaoshughulikia hali ya Niger.

Blinken amesema Marekani bado inaona kuwa ni "muhimu" kwamba viongozi wa mapinduzi nchini Niger kumuachilie rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum, na familia yake kutoka kizuizini, na kwamba Niger inapaswa kurejea katika utaratibu wa katiba.

Kwa ajili hiyo, Marekani "inaunga mkono sana kile ECOWAS inachofanya," amesema.

Kuhusu kama Marekani itaunga mkono matumizi ya nguvu yanayotishiwa na ECOWAS, Blinken amesema "sitatangulia mbele zaidi ya tulipo sasa au kuingia katika dhana zozote kuhusu kile kinachoweza kutokea katika siku zijazo."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha