

Lugha Nyingine
Wakuu wa kijeshi wa Afrika Magharibi kujadili mzozo wa Niger wiki hii
(CRI Online) Agosti 16, 2023
Wakuu wa kijeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) watakutana nchini Ghana wiki hii kujadili uwezekano wa kuingilia kati mzozo wa Niger.
Mkutano huo wa Alhamisi na Ijumaa, ambao awali ulipangwa kufanyika wikendi iliyopita lakini ukaahirishwa, unafanyika baada ya viongozi wa ECOWAS wiki iliyopita kuidhinisha kutumwa kwa "kikosi cha kuwa tayari ili kurejesha utulivu wa kikatiba" nchini Niger, ambayo rais wake alipinduliwa Julai 26.
Mkutano wao wa kilele uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja Alhamisi ya wiki iliyopita, pamoja na kutangaza kuwa na kikosi hicho cha utayari pia ulithibitisha haja ya jumuiya hiyo kupata suluhu ya kidiplomasia.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma