Wang Yi ahutubia ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya China na Asia Kusini

(CRI Online) Agosti 17, 2023

Mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Yi amehudhuria na kuhutubia hafla ya ufunguzi wa maonesho ya saba kati ya China na nchi za Asia ya kusini yanayofanyika mjini Kunming, mkoani Yunnan kusini magharibi mwa China.

Kwenye hotuba yake hiyo Bw. Wang amesema, mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 10 tangu kuanzishwa maonesho hayo, pia ni maadhimisho ya kutimia miaka 10 tangu kutolewa kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na wazo la kidiplomasia la ujirani mwema linalojumuisha upendo, udhati, kunufaishana na ujumuishaji.

Wang amebainisha kuwa katika miaka 10 iliyopita, pande husika zimeimarisha mshikamano na ushirikiano katika kulinda usalama wa kikanda na mazingira ya maendeleo. Pia zimeendelea kujenga Ukanda Mmoja, Njia Moja na kupata mafanikio makubwa katika muunganisho, miundombinu, biashara na uwekezaji, na sekta nyingine. Halikadhalika zimefanya mabadilishano ya kina ya kirafiki, kufuata kanuni ya uwazi na ujumuishaji, na kujenga jukwaa la ngazi mbalimbali la mabadilishano kati ya watu.

Amesisitiza kwamba, China iko tayari kushirikiana na nchi za Asia ya kusini katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuhimiza nguvu mpya za maendeleo, kujenga jumuiya yenye maendeleo ya pamoja, na kutoa mchango katika kudumisha amani, utulivu na ustawi wa kanda hiyo.

Waziri Mkuu wa Sri Lanka Bw. Dinesh Gunawardena, Makamu wa Rais wa Laos Pany Yathotou, Makamu wa Rais wa Nepal Ram Sahay Prasad Yadav, na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bw. Tran Luu Quang walihudhuria ufunguzi huo.

(Picha inatoka CRI.)

(Picha inatoka CRI.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha