

Lugha Nyingine
Watu 19 waokolewa katika operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa kikosi cha ADF
Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) na Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC (FARDC) katika operesheni yao ya pamoja yamewaokoa watu 19 waliokuwa wametekwa nyara na waasi wa Kundi la The Allied Democratic Forces (ADF) katika Jimbo la Ituri nchini DRC linalopakana na Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meja Bilal Katamba, afisa habari za umma wa Kitengo cha Mlimani cha UPDF, waliookolewa ni pamoja na watoto wanane, wanawake tisa na wanaume wawili, ambao waliripoti siku ya Jumamosi iliyopita katika kambi ya pamoja ya Bwakadde iliyoko Ituri baada ya majeshi hayo kushambulia kituo cha ADF katika vilima vya Tingwe, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Erengeti ya DRC.
Taarifa hiyo pia imesema, watu hao 19 wamesafirishwa kwa ndege na UPDF na kupatiwa matibabu na timu ya madaktari wa UPDF. Majeshi hayo yanaendelea kuwasaka waasi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma