Mjumbe wa Umoja wa Mataifa asema utulivu wa Libya ni muhimu kwa usalama wa kikanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023

Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Agosti 22, 2023. (Loey Felipe/Picha za UN/ Xinhua)

Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Agosti 22, 2023. (Loey Felipe/Picha za UN/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesema siku ya Jumanne kwamba ni muhimu kwa kurejesha utulivu wa Libya ili kulinda usalama wa kikanda.

Amesema, kudumisha utulivu wa Libya ni jambo la muhimu zaidi kwa sasa kutokana na matukio yaliyotokea hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na mapigano ya hivi karibuni huko Tripoli, pamoja na msukosuko wa kikanda nchini Sudan na Niger.

"Matukio ya sasa nchini Libya na katika kanda hiyo yanaonyesha kuwa mipango ya mpito imejaa hatari za ghasia na mgawanyiko kwa nchi," Bathily amesema kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Amebainisha kwamba, bila makubaliano ya kisiasa yaliyo jumuishi ambayo yanafungua njia kwa uchaguzi wa amani, ulio jumuishi na wenye uwazi kote nchini Libya, hali itakuwa mbaya zaidi na kusababisha mateso zaidi kwa watu wa Libya.

"Kwa hiyo natoa wito kwa viongozi wote kuchukua wajibu wa kisiasa na kimaadilikukomesha mipango ya mpito isiyo na kikomo, kuvunja hali ya kukwama uliopo na kuacha kukatisha tamaa matarajio halali ya Walibya kuhusu uchaguzi, amani na ustawi," amesema.

Libya ilishindwa kufanya uchaguzi mkuu Mwezi Desemba, Mwaka 2021 kama ilivyopangwa hapo awali, kwa sababu ya kutokubaliana juu ya sheria za uchaguzi kati ya pande husika za Libya.

Tangu kuangushwa kwa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi Mwaka 2011, nchi hiyo imekuwa ikijitahidi kuhamia kwenye utawala wa kidemokrasia huku kukiwa na ongezeko la ghasia na mgawanyiko wa kisiasa.

Kwenye hotuba yake hiyo kwa Baraza la Usalama, huku akitoa wito wa kuepuka maamuzi ya upande mmoja kwa gharama yoyote ile, Bathily amesisitiza kwamba masuala yote yanayohusiana na uchaguzi nchini Libya yanapaswa kutatuliwa kupitia majadiliano na maelewano kati ya wahusika wote.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha