Matumizi ya mianzi yahimizwa kama mbadala endelevu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023

Wanafunzi kutoka Guinea wakihudhuria warsha kuhusu ufumaji wa mianzi iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mianzi na Migazi huko Meishan, Mkoa wa Sichuan, China siku ya Jumanne. (Yao Yongliang/China News Service)

Wanafunzi kutoka Guinea wakihudhuria warsha kuhusu ufumaji wa mianzi iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mianzi na Migazi huko Meishan, Mkoa wa Sichuan, China siku ya Jumanne. (Yao Yongliang/China News Service)

Shirika la Kimataifa la Mianzi na Migazi INBAR)limekuwa likihimiza matumizi ya mianzi nchini India, likichangia maendeleo endelevu na uhimilivu wa kiuchumi nchini humo.

India, mwanachama wa INBAR tangu mwaka 1998, imeshuhudia utambuzi wa spishi zaidi ya 130 za mianzi nchini humo. Kwa kutambua uwezezo mkubwa wa mianzi kama rasilimali muhimu, INBAR imekuwa ikifanya kazi kutumia kikamilifu mmea huu unaoweza kutumimika katika sekta mbalimbali kama vile ujenzi, zana za kilimo, samani, ala za muziki, bidhaa za chakula, na kazi za mikono.

Shirika hilo limekuwa likihamasisha matumizi ya mianzi kama mbadala wa plastiki zinazotumiwa kwa mara moja. Imeelezwa kwamba kwa ukuaji wake wa haraka, ustahimilivu na uendelevu, mianzi inaweza kuchukua nafasi ya plastiki katika matumizi mbalimbali. Hii ni pamoja na uzalishaji wa vikombe, mirija ya kunywea vinywaji, karatasi, na ufungashaji, vyote hivi vinaweza kuchakatwa na ni rafiki kwa mazingira.

Mwaka jana, Mpango wa Kutumia Mianzi Kama Mbadala wa Plastiki ulizinduliwa katika Majadiliano ya Ngazi ya Juu kuhusu Maendeleo ya Kimataifa pembezoni mwa Mkutano wa 14 wa viongozi wakuu wa nchi za ushirikiano wa Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) uliofanyika kwa njia ya mtandao mjini Beijing, China.

Kwa kuhimiza matumizi ya mianzi, INBAR inalenga kupambana na athari mbaya kwa mazingira zinazosababishwa na plastiki zinazotumiwa kwa mara moja. Plastiki hizi, zinazotengenezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mafuta ya kisukuku, zinaleta hatari kubwa kwa afya ya binadamu kwani huharibu na kuwa vipande vidogo vya plastiki na kuathiri vyanzo vya chakula.

Ikiwa ilianzishwa Mwaka 1997, INBAR imekuwa na jukumu muhimu katika kuhimiza ushirikiano wa Kusini-Kusini. Inahimiza maendeleo endelevu yaliyo rafiki kwa mazingira kupitia matumizi ya rasilimali za mianzi na migazi. Shirika hilo lina makao yake makuu nchini China na moja ya ofisi zake tano za kikanda nchini India. Kupitia ahadi yake kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini, INBAR imechangia kukuza ushirikiano, ubadilishanaji maarifa, na maendeleo endelevu kati ya nchi wanachama wake.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha