Ushirikiano wa ujuzi kati ya nchi za BRICS wasaidia kuondoa umaskini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023

Mfanyakazi akionesha mbegu za mahindi kwenye kiwanda cha mbegu cha Kampuni ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya Longping ya Brazil huko Jardinopolis, Brazil mwezi wa Machi. Kikiwa kimewekezwa na China na kupewa jina la mtaalamu maarufu wa nafaka wa China, kampuni hiyo inashughulika na kuendeleza mbegu zinazofaa kwa hali ya hewa na udongo wa Brazil. (Picha imepigwa na Wang Tiancong/Xinhua)

Watafiti na mafundi zaidi ya 700 kutoka sekta ya kilimo ya Afrika Kusini mwezi uliopita walishiriki kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na Baraza la Utafiti wa Sayansi za Binadamu la nchi hiyo na Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China.

Katika shughuli hiyo ya siku tatu, upande wa China ulieleza namna utaalamu ulivyosaidia wakulima waliokuwa maskini kuhamia katika kupanda mazao yenye thamani nyingi zaidi, na kupata ustawi wa kiuchumi. Walitoa simulizi kuhusu kukuza tasnia ya uyoga wa kuvu kwa mafanikio kwenye Mkoa wa uzalishaji zao la ngano wa Shaanxi, ili kuongeza kipato cha wakulima vijijini kama mojawapo wa mifano kuelezea hoja yao. Walisema, mafundi hao wa kilimo, ambao wanaufahamu wa kina wa mbinu za kilimo na habari za soko wana jukumu kubwa la kufanya katika kupambana na umaskini vijijini.

Shughuli hiyo ni moja ya miradi ya mafunzo inayozidi kuongezeka kwa idadi inayoandaliwa na China na Afrika Kusini kwa ajili ya kuhimiza mabadilishano ya maarifa katika kilimo na udhibiti wa umaskini. Nchi hizo zote ni wanachama wa kundi la BRICS, kundi la nchi zinazoongoza duniani zenye uchumi unaoibuka, ambalo pia linahusisha Brazil, Russia na India.

Uhamishaji wa maarifa kati ya China na Afrika Kusini ni mfano wa mipango mingine ya aina hii inayotekelezwa na China na nchi nyingine za BRICS, ambazo zinachukua asilimia 42 ya idadi ya watu wote duniani.

Hadi mwisho wa Mwaka 2021, China imesaidia kufundisha mafundi wa kilimo, wataalam wa usimamizi, na wanafunzi wa shahada ya uzamili na uzamivu zaidi ya 350 wa Afrika Kusini, takwimu rasmi zinaonesha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha