Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China: Hatutaki Tarehe 24 Agosti, 2023 Iwe Siku ya  Balaa ya Mazingira ya Bahari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023

Katika mkutano na waandishi wa habari wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China tarehe 23 mwezi huu, msemaji Wang Wenbin alipoulizwa kuhusu serikali ya Japani kutangaza kutiririsha maji machafu ya kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi baharini kuanzia tarehe 24, alisema kwamba China haitaki siku hiyo iwe siku ya balaa kwa mazingira ya bahari.

Kama Japani ikitekeleza mpango huo bila ya kujali upinzani, ni lazima ibebe jukumu la kihistoria, alisema Wang.

Wang alisema, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Sun Weidong tarehe 22 alimwita Balozi wa Japan nchini China Chiaki Takahashi, ambapo alieleza upinzani mkali wa China kwa upande wa Japan. . Upande wa China umedhihirisha kuwa, serikali ya Japan imepuuza malalamiko makali na upinzani mkubwa wa jumuiya ya kimataifa ikishikilia kutangaza kuanzisha mpango wake wa kutiririsha maji machafu ya nyuklia baharini. Hatua hiyo ya kuhamisha wazi hatari ya kuenea kwa uchafu wa nyuklia hadi katika nchi jirani ikiwemo China na jumuiya ya kimataifa, na imeweka maslahi yake binafsi juu ya maslahi ya muda mrefu baadaye ya watu wa nchi nyingine mbalimbali duniani . Hiki ni kitendo cha ubinafsi kisichowajibika kabisa. China inakifuatilia kwa umakini zaidi na kukipinga vikali.

Wang alisema,"Bahari ni maskani ya buluu yanayotegemewa na binadamu wote, na hauruhusiwi upande wa Japan kutiririsha ovyoovyo maji machafu ya nyuklia baharini. Upande wa Japan unashikilia kutekeleza mpango wake huo hakika inachukulia mazingira ya bahari ya dunia na afya ya binadamu wote kama dau lake .” Alisema, kama upande wa Japan una udhati wa kuondoa wasiwasi wa nchi jirani zake, unapaswa kusitisha mpango huo mara moja na kushiriki katika mazungumzo bila kuweka masharti, ili kujadili vya kutosha masuluhisho yote salama yenye uwezekano.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha