Rais Xi asema kuwa maendeleo ya kisasa ya China yataleta fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Mfumo wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Mfumo wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

JOHANNESBURG - China inaendeleza maendeleo yake ya kisasa yenye kiwango cha juu, ambayo yataleta fursa mpya za ushirikiano kati ya China na Ethiopia, amesema Rais wa China Xi Jinping hapa Jumatano.

“China ni rafiki wa kutegemewa na mshirika wa kweli wa Ethiopia,” Rais Xi amesema alipokutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS.

Ameeleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimedumisha mabadilishano na mawasiliano ya mara kwa mara ya ngazi ya juu, na zimepata matokeo ndani ya mifumo ya ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

“China inatilia maanani sana uhusiano wake na Ethiopia na kuunga mkono mchakato wake wa amani, maendeleo na ustawishaji wa taifa,” Rais Xi amesema na kuongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na Ethiopia ili kuhimiza mabadilishano ya pande mbili na kupanua ushirikiano wa pande zote, ili urafiki wa pande hizo mbili uweze kufurahia kuungwa mkono zaidi na watu wengi na ushirikiano wa kiwenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ethiopia uweze kushuhudia maendeleo zaidi.

Pamoja na kusisitiza pande hizo mbili kuunganisha mipango yao ya kitaifa ya maendeleo hasa kwa kutaja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Reli ya Addis Ababa-Djibouti, Rais Xi amesema, China iko tayari kushirikiana na Ethiopia katika kuhimiza utekelezaji wa Mtazamo wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika na kutoa mchango kwa ajili ya amani na utulivu wa kanda hiyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Abiy amesema, urafiki kati ya Ethiopia na China ni mkubwa na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa vizuri. Ameshukuru China kwa kuiunga mkono Ethiopia kwa muda mrefu.

Amesema, Ethiopia inatarajia kujiunga na BRICS ili kusukuma mbele ushirikiano wa karibu katika mifumo ya kimataifa na kufungua mustakabali mzuri zaidi wa pamoja wa nchi hizo mbili. 

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 15 wa Wakuu waBRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 15 wa Wakuu wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha