Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais wa Senegal Macky Sall mjini Johannesburg

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Senegal Macky Sall  katika wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

JOHANNESBURG - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Senegal Macky Sall siku ya Jumatano katika wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Rais Xi amesema, Senegal ni mshirika muhimu wa China barani Afrika, kutokana na juhudi za pamoja katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimekuwa na hali ya kuaminiana kisiasa na ushirikiano wenye manufaa katika sekta mbalimbali.

Amesema China inaunga mkono kithabiti juhudi za Senegal katika kulinda utulivu na maendeleo ya nchi, China iko tayari kuimarisha kuungana mkono na Senegal na kuzidisha ushirikiano katika sekta kama vile viwanda, kilimo, miundombinu na rasilimali watu, kulinda kwa pamoja haki yao halali ya maendeleo na kusukuma maendeleo zaidi ya uhusiano wao wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Amesisitiza kuwa hivi sasa, hali ya kimataifa inapitia mabadiliko makubwa na yenye changamano, na kwamba China na Afrika zinahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote kuimarisha mshikamano na ushirikiano.

Rais Xi amesema China inaunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na Kundi la nchi 20, na iko tayari kubadilishana na ndugu wa Afrika uzoefu na fursa zake za maendeleo, kuendelea kufuata kanuni za udhati, matokeo halisi, urafiki na uaminifu, kutafuta maslahi makubwa zaidi na maslahi ya pamoja, na kusukuma mbele utafutaji wa pamoja wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Zikiwa wenyeviti wenza wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), China na Senegal zimesaidiana, kushirikiana na kufanikiwa kufanya shughuli muhimu mfululizo ikiwa ni pamoja na Mkutano Maalum wa China na Afrika kuhusu Mshikamano dhidi ya UVIKO-19, alisema.

Kwa upande wake, Rais Sall amesema kuwa Senegal na China ni washirika wa kimkakati wa hali ya juu, akimsifu Rais Xi kama rafiki mkubwa wa Afrika na Senegal.

Ameishukuru China kwa kuongoza katika kuunga mkono hadharani AU kujiunga na Kundi la nchi 20, akisema kuwa nchi yake, ikiwa ni mwenyekiti mwenza wa FOCAC, itaendelea kuwasiliana kwa karibu na kushirikiana na China ili kuhimiza maendeleo zaidi ya uhusiano wa Afrika na China. 

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Senegal Macky Sall  katika wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Senegal Macky Sall katika wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha