Hotuba ya Rais Xi wa China kwenye mkutano wa kufungwa wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS yamepata uitikio kwenye jumuiya ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023

Mchana wa Tarehe 22, Agosti kwa saa za huko, Rais Xi Jinping alitoa hotuba kwenye mkutano wa kufungwa wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS 2023.

Watu wa kimataifa waliohojiwa na waandishi wa habari wa People’s Daily walisema kuwa hotuba ya Rais Xi Jinping ilielekeza njia kwa pande zote za kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na ilitia imani na msukumo katika kuimarisha zaidi maendeleo ya wazi ya kimataifa, ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja na ushirikiano wa nchi za BRICS.

Inaonesha moyo wa BRICS wa uwazi na jumuishi,ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Masuala ya China cha Brazil Ronnie Lins alisema kuwa upande wa China imetoa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia,Pendekezo la Usalama wa Dunia, Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, yote hayo ni muhimu sana katika kuhimiza maendeleo endelevu, kulinda amani na usalama wa kimataifa, na kuhimiza mawasiliano kati ya ustaarabu mbalimbali na kufundishana, na yatasaidia nchi kuendeleza mchakato wao wa ujenzi wa mambo ya kisasa na kupata maendeleo na ustawi kwa pamoja.

Boris Guseletov, mtafiti mwandamizi katika Ofisi ya Utafiti wa Ulaya ya Taasisi ya Sayansi ya Russia, alisema kuwa zikiwa wawakilishi wa nchi zenye masoko yanayojitokeza na nchi zinazoendelea, nchi za BRICS zinafanya kazi yake muhimu zaidi katika kudumisha amani na utulivu wa dunia.

Kutoa msukumo kwa ushirikiano kati ya nchi zenye masoko yanayojitokeza na nchi zinazoendelea

Stavros Nicolau, mwakilishi wa Afrika Kusini wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS, alisema tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ushirikiano wa BRICS, thamani ya biashara kati ya nchi wanachama imepata ongezeko dhahiri. Kuanzia Mwaka 2017 hadi 2021, thamani ya biashara kati ya Afrika Kusini na nchi nyingine za BRICS iliongezeka kwa 44%. "Afrika Kusini ingependa kujenga daraja kati ya nchi za BRICS na bara la Afrika, na kufanya kazi pamoja na nchi mbalimbali katika kutoa msukumo kwa ushirikiano wa nchi za masoko yanayojitokeza na nchi zinazoendelea."

Baloo Demisi, mtafiti wa sera katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Ethiopia, alisema kuwa nchi nyingi zina shauku kubwa ya kujiunga na mfumo wa ushirikiano wa BRICS. Kwa kubadilishana uzoefu, kutoa msaada na kuhimiza ushirikiano, na nchi za BRICS zinaungana na nchi nyingine zinazoendelea katika kukuza maendeleo ya dunia. Mfumo huu wa ushirikiano una umuhimu mkubwa katika kujenga utaratibu wa usawa na halali wa kimataifa, kuimarisha ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia nzima.

Kuleta fursa nyingi zaidi kwa uwazi na maendeleo ya dunia, ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja

"Tangu kufanyika kwa mageuzi na kufungua mlango katika miaka zaidi ya 40 iliyopita, mabadiliko makubwa sana yametokea nchini China, ambayo yameonyesha msukumo mkubwa wa uwazi na ushirikiano." Mtendaji Mkuu wa Kundi la Numolux ya Afrika Kusini, Hilton Klein alisema China imeanzisha ushirikiano wa karibu na nchi mbalimbali katika uvumbuzi na utafiti wa teknolojia, ili kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya teknolojia.

"Hotuba ya Rais Xi Jinping imewatia moyo sana watu wanaoshughulikia kazi za viwanda na biashara wa kimataifa." Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Biashara ya Gordon katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini, Farhana Palukh alisema, " China ikiwa nchi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi wake, uchumi wa China una uwezo mkubwa wa kustahimili matatizo, nguvu kubwa na uhai wa kutosha, na hali yake ya msingi ya kuendelea vizuri haitabadilika katika muda mrefu. Hii inaleta imani kwa uchumi wa dunia unaofufuka."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha