

Lugha Nyingine
Viongozi wa Nchi za BRICS watoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali na kulinda uhusiano wa pande nyingi
Mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefanyika Johannesburg, Afrika Kusini siku ya Jumatano kuanzia Asubuhi kwa saa za Cape Town na kuongozwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini. Rais Xi Jinping wa China, Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Waziri Mkuu wa Hindi Narendra Modi, na Rais Vladimir Putin (kwa kupitia video) wameshiriki kwenye mkutano huo.
Kwenye hotuba zao katika mkutano huo, viongozi hao wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kifedha, kupanua ushirikiano wa kiusalama na kisiasa, kuhimiza mabadilishano kati ya watu na ya kitamaduni, kuboresha mfumo wa uongozi wa dunia na kulinda uhusiano wa pande nyingi.
Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini, ambaye anashikilia nafasi ya mwenyekiti wa zamu wa nchi za BRICS, kwenye hotuba yake amesema kuwa, katika miongo iliyopita, nchi za BRICS zimekuwa nguvu muhimu ya kusukuma ongezeko la uchumi, biashara na uwekezaji duniani. Amesema, nchi za BRICS zinahamasisha ujumuishaji, na kuhimiza ujenzi wa utaratibu wa dunia ambao ni wenye haki na mantiki zaidi. Ameeleza kuwa, hali halisi mpya ya uchumi, siasa, jamii na teknolojia inataka nchi ziimarishe ushirikiano kati yao.
Rais Lula wa Brazil amesema kwenye hotuba yake kuwa ndani ya miaka michache tu, dunia imerudi nyuma kutoka hali nzuri ya kuwa na Dunia yenye nchi nyingi zenye nguvu sawa hadi kwenye hali ambayo mawazo yaliyopitwa na wakati ya Vita Baridi na mashindano ya siasa za kijiorojia vinarejea. Amesema, hali hiyo italeta ukosefu mkubwa wa hali ya kuwa na uhakikia na kuharibu uhusiano wa pande nyingi, na hatari zinazohusika hazikubaliki kwa binadamu. Ametoa wito wa kurejesha mfumo wa biashara wa pande nyingi kwa ajili ya “biashara yenye haki, kutabirika, usawa na ya bila ubaguzi”.
Rais Putin wa Russia siku hiyo alitoa hotuba kwa njia ya video. Putin amesema, nchi za BRICS zimeongeza uwezo wao mwaka hadi mwaka, na zimekuwa mfumo muhimu kwenye jukwaa la Dunia huku ushawishi wao wa mambo ya kimataifa ukiongezeka mara kwa mara. Amesema kwamba, Russia inaunga mkono kuimarisha ushirikiano katika uvumbuzi wa kimataifa, mageuzi ya kidijitali na akili bandia, elimu ya ufundi, na mambo ya wanawake.
Waziri Mkuu wa India Modi amesema kwenye hotuba yake kwamba, katika miongo miwili iliyopita, nchi za BRICS zimepata mafanikio mengi, na Benki Mpya ya Maendeleo imefanya kazi muhimu katika maendeleo ya “Ulimwengu wa Kusini”. Kupitia ushirikiano wa safari za anga ya juu, kuanzisha kituo cha utafiti na uzalishaji chanjo na miradi mingine, mfumo wa ushirikiano wa BRICS unaleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu wa kawaida katika nchi hizo. Modi amependekeza nchi hizo kuimarisha ushirikiano zaidi katika safari za anga ya juu, elimu, teknolojia, matibabu ya jadi na nyanja nyingine. Modi amesema, India inaunga mkono kuongeza nchi wanachama wapya wa BRICS, na kukaribisha makubaliano na hatua zaidi za maendeleo katika hili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma