Mkuu wa Jeshi la Kibinafsi la Wagner afariki katika ajali ya ndege karibu na Moscow, Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023

Picha iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Russia Agosti 23, 2023 ikionyesha eneo la ajali ya ndege ya kibinafsi katika Eneo la Tver karibu na Moscow, Russia. (Kamati ya Uchunguzi ya Russia/ Xinhua)

Picha iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Russia Agosti 23, 2023 ikionyesha eneo la ajali ya ndege ya kibinafsi katika Eneo la Tver karibu na Moscow, Russia. (Kamati ya Uchunguzi ya Russia/Xinhua)

MOSCOW/WASHINGTON - Shirika la Usafiri wa Ndege na Uchukuzi la Russia limethibitisha Jumatano kwamba kiongozi wa Jeshi la Kibinafsi la Wagner Yevgeny Prigozhin amefariki katika ajali ya ndege iliyotokea eneo la Tver karibu na Mji wa Moscow.

Kwa mujibu wa orodha ya majina iliyotolewa na shirika hilo kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Telegram, Prigozhin alikuwa miongoni mwa watu kumi waliopoteza maisha katika ajali hiyo mapema Jumatano.

Shirika hilo limesema mapema ya Jumtano kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusu chanzo cha ajali ya ndege hiyo katika Eneo la Tver, na kubainisha kuwa Yevgeny Prigozhin alikuwa miongoni mwa abiria.

Wizara ya Hali ya Dharura ya Russia imesema, Ndege ya kibinafsi ya Embraer iliyokuwa ikitoka Moscow kuelekea St. Petersburg ilianguka katika Eneo la Tver siku ya Jumatano, na watu wote kumi waliokuwemo wamefariki katika ajali hiyo.

Kundi la waandishi wa habari la Ikulu ya Marekani limesema, Rais wa Marekani Joe Biden amesikiliza ripoti kuhusu habari zilizosema ndege iliyombeba Prigozhin imeanguka nchini Russia.

"Sijui kwa kweli kilichotokea lakini sishangai," Biden amesema alipoulizwa kuhusu ajali hiyo. Rais Biden, akiwa katika Jimbo la Nevada siku hiyo bila shughuli za umma zilizopangwa, amesema alikuwa akifanya mazoezi ya mwili wakati alipoambiwa juu ya habari hiyo.

"Tumeona ripoti hizo. Ikithibitishwa, hakuna anayepaswa kushangaa," Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Marekani Adrienne Watson amesema kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kwa jina la Twitter.

Picha iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Russia Agosti 23, 2023 ikionyesha eneo la ajali ya ndege ya kibinafsi katika Eneo la Tver karibu na Moscow, Russia. (Kamati ya Uchunguzi ya Russia/ Xinhua)

Picha iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Russia Agosti 23, 2023 ikionyesha eneo la ajali ya ndege ya kibinafsi katika Eneo la Tver karibu na Moscow, Russia. (Kamati ya Uchunguzi ya Russia/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha