Rais Xi Jinping asema upanuzi wa BRICS ni tukio la kihistoria, mwanzo mpya wa ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2023

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023. Viongozi wa BRICS wamekubaliana Alhamisi kualika nchi sita, ambazo ni Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kujiunga na kundi hilo. (Xinhua/Ding Haitao)

JOHANNESBURG - Rais wa China Xi Jinping amesema kwamba upanuzi wa BRICS ni tukio la kihistoria na ni mwanzo mpya wa ushirikiano wa BRICS.

Rais Xi ameyasema hayo siku ya Alhamisi katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) baada ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kutangaza kuwa nchi sita ambazo ni Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimealikwa kuwa wanachama wapya wa BRICS.

“China inatoa pongezi zake kwa nchi hizi, na kushukuru kwa juhudi zinazofanywa na Afrika Kusini, mwenyekiti wa BRICS na Rais Ramaphosa,” Rais Xi amesema.

Amesisitiza kuwa, upanuzi huo unaonyesha azma ya nchi za BRICS ya kuungana na kushirikiana na nchi nyingine zinazoendelea, unakidhi matarajio ya jumuiya ya kimataifa, na kuchangia maslahi ya pamoja ya nchi zenye masoko yanayoibukia na nchi zinazoendelea.

Ameongeza kuwa upanuzi huo pia utaingiza nguvu mpya katika utaratibu wa ushirikiano wa BRICS, na kuimarisha zaidi nguvu za amani na maendeleo ya dunia.

“Nchi za BRICS zote zina ushawishi na zinabeba wajibu muhimu kwa amani na maendeleo ya dunia,” Rais Xi amesema.

Rais Xi ameeleza kuwa, wakati wa mkutano huu, majadiliano ya kina yalifanyika kuhusu hali ya sasa ya kimataifa na ushirikiano wa BRICS. “Makubaliano mapana yamefikiwa, taarifa imetolewa, na matokeo yenye tija kufikiwa,” amesema.

Rais Xi amesema anaamini kuwa maadamu nchi za BRICS zinaungana, mengi yanaweza kupatikana katika ushirikiano wa BRICS, na mustakabali mzuri unangojea nchi za BRICS.

Ametoa wito kwa nchi wanachama wa BRICS kufanya kazi pamoja kufungua ukurasa mpya wa mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zenye masoko yanayoibukia na nchi zinazoendelea kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo na waandishi wa habari uliandaliwa na Rais Ramaphosa, na kuhudhuriwa pia na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Rais wa Russia Vladimir Putin alishiriki mtandaoni.

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha