Xi Jinping akutana na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2023

Asubuhi ya tarehe 24, Agosti kwa saa za Johannesburg, Rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Samia Suluhu Hasaan wa Tanzania  katika wakati wa Mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha ilipigwa na Xie Huanchi/Xinhua)

Asubuhi ya tarehe 24, Agosti kwa saa za Johannesburg, Rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Samia Suluhu Hasaan wa Tanzania katika wakati wa Mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha ilipigwa na Xie Huanchi/Xinhua)

Asubuhi ya tarehe 24, Agosti kwa saa za Johannesburg, rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania wakati wa mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Xi alisema, rais Samia aliwasili China mwezi Novemba mwaka jana, ambapo ulikuwa wakati mzuri zaidi wa uhusiano kati ya China na Tanzania. Makubaliano yaliyofikiwa wakati huo yanatekelezwa kwa juhudi na ufanisi. Siku zote ushirikiano wa nchi hizo mbili umekuwa safu ya mbele ya ushirikiano wa China na Afrika, na reli ya TAZARA ni kumbukumbu nzuri ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili. Mwaka ujao utatimia miaka 60 tangu China na Tanzania zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia, upande wa China ungependa kutumia fursa hii ya maadhimisho, kuendelea kushikilia kuungana mkono na upande wa Tanzania juu ya maslahi ya kimsingi ya kila upande wao na masuala muhimu yanayofuatiliwa zaidi nazo, na kuimrisha ushirikiano wa kimkakati. Kwenye hali ya kimataifa ya hivi sasa, kuimarisha ushirikiano wa China na Afrika kunanufaisha mshikamano wa nchi zinazoendelea na maslahi yao halali ya maendeleo.

Rais Samia alisema, anafurahia sana mafanikio ya ziara yake nchini China mwaka jana, ambapo yeye na rais Rais Xi walipandisha pamoja uhusiano kati ya Tanzania na China kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote. Nchi hizo mbili zinadumisha mawasiliano ya karibu kwenye ngazi mbalimbali, miradi yao ya ushirikiano inatekelezwa vizuri. Upande wa Tanzania unasifu sana uungaji mkono na msaada uliotolewa na upande wa China kwa maendeleo ya nchi zinazoendelea, na Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea zimenufaika na “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na mapendekezo mengine ya rais Xi. Tanzania inatarajia mwaka ujao kusherehekea pamoja na upande wa China maadhimisho ya miaka 60 uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hizo mbili, na kuinua zaidi kiwango cha maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha