MAONI: Utirirshaji wa Japan wa maji machafu ya nyulia baharni ni ubinafsi nakutowajibika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2023

Watu wakiwa wamekusanyika huko Busan, Korea Kusini, Agosti 24, 2023, kupinga uamuzi wa Japan wa kutiririsha baharini maji machafu yenye mionzi ya nyuklia. (NEWSIS kupitia Xinhua)

Watu wakiwa wamekusanyika huko Busan, Korea Kusini, Agosti 24, 2023, kupinga uamuzi wa Japan wa kutiririsha baharini maji machafu yenye mionzi ya nyuklia. (NEWSIS kupitia Xinhua)

BEIJING - Jumuiya ya kimataifa inapaswa kushtushwa na kitendo cha Japan cha kutiririsha maji machafu ya nyuklia kwenye bahari yetu ya pamoja, na nchi hiyo lazima ihimizwe kufikiria upya hatua hii isiyo ya haki na ya kutowajibika.

Serikali ya Japan, bila kujali ukosoaji na upinzani mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, kwa uamuzi wa kibabe wa upande mmoja imeanza kutiririsha maji hayo machafu ya nyuklia ya Fukushima ndani ya bahari siku ya Alhamisi.

Kama Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alivyosema, athari zake zinaenda nje ya mipaka ya Japan, na suala hilo siyo suala la kibinafsi kwa Japan.

Ajali ya Kinu cha nyuklia cha Fukushima Daachi ni mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya nyuklia duniani hadi sasa. Kwa hiyo, maji hayo yanajulikana kuwa na vipengele zaidi ya 60 vya mionzi, vinavyojulikana kama radionuclides, hali ambayo inafanya utiririshaji wake kuwa tofauti kabisa na uendeshaji wa kawaida wa mashine za nyuklia.

Hakuna teknolojia inayoweza kutumika kutibu wingi kama huo wa nyuklides ipasavyo, na vimelea fulani vya muda mrefu vinaweza kutawanyika kupitia mikondo ya bahari, na kusababisha athari zisizotarajiwa kwa ikolojia ya baharini na afya ya binadamu.

Mfumo wa Hali ya Juu wa Kushughulikia vimiminika (ALPS), ambacho ni kituo kikuu cha Japan cha kushughulikia maji machafu ya nyuklia kilichoanza kufanya kazi kwa majaribio mnamo Machi 2013, kilikumbwa na hitilafu mara kwa mara. Dunia inahitaji kujua jinsi ya kuhakikisha ufanisi na kutegemewa kwa ALPS kadri kituo kinavyozeeka.

Siyo tu kiwango cha maji hayo machafu ya nyuklia kwenye kituo hicho ni kikubwa na muundo wake ni changamano, lakini muda wa utiririshaji wake utadumu kwa muda usio na kifani.

Kukosekana kwa uaminifu na tathmini ya kisayansi kumesababisha mashaka juu ya mantiki ya mpango wa Japan wa kutiririsha maji hayo kwa miaka 30, na kuendelea na mpango huo kwa upande bila ushirikiano wa dhati wa kimataifa kumeweka mfano hatari zaidi wakati ambapo sayari, haswa bahari zake, zinakabiliwa na changamoto na vitisho vingi.

Japani "inahalalisha" mpango wake huo kwa kutumia kigezo cha tathmini pekee ya usalama iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), lakini tathmini hiyo ina mapungufu yaliyo dhahiri na inakabiliwa na madai ya upendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha