

Lugha Nyingine
Msomi wa Tanzania: nchi za Afrika zatakiwa kuhamasishwa kujiunga na mfumo wa BRICS
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi.(Picha na mhojiwa)
Mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti huko Johannesburg, Afrika Kusini, kaulimbiu ya mkutano huo ni “BRICS na Afrika: kuimarisha uhusiano wa wenzi, kuhimiza ongezeko kwa kila upande, kutimiza maendeleo endelevu, kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi wa kijumuishi”. Katika mahojiano na waandishi wa habari wa Gazeti la People's Daily Online hivi karibuni, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Tanzania, Humphrey Moshi alisema kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kutumia mifumo ya ushirikiano wa kimataifa kama BRICS kujinufaisha, na nchi za Afrika zinatakiwa kuhamasishwa kujiunga na mfumo wa BRICS.
Hivi sasa, hali ya kimataifa inabadilika sana, na mgogoro kati ya Russia na Ukraine umeathiri vibaya uchumi wa Afrika, hasa sekta ya nafaka inayowakilishwa na ngano na mafuta ya kupikia. Bara la Afrika linakabiliwa na matatizo ya mfumuko wa bei na usalama wa chakula.
Moshi alisema kuwa kama nchi za Afrika zikitumia vizuri majukwaa ya kimataifa yakiwemo BRICS, kasi za maendeleo yao zitaongezeka kwa ufanisi. "Ni dhahiri kwamba hivi sasa sekta ya viwanda imepata ongezeko lenye nguvu, hivyo ni lazima kuongeza uwekezaji kwenye kilimo, kwa kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Afrika na familia za waafrika zinazochukua asilimia 64 zinategemea kilimo kwa maisha yao ya kila siku."
Akizungumzia umwamba wa dola ya Kimarekani, alisema kuwa kuongeza thamani ya dola ya Kimarekani kunaweza kusababisha mfumuko wa bei katika nchi husika na kupunguza uwezo wao wa kukopa na kulipa madeni. " Kama nchi wanachama wa BRICS zinaweza kutumia njia mbadala ya dola ya Kimarekani kufanya biashara, hii itakuwa ni fursa kwa nchi za Afrika."
Alipotaja ushirikiano kati ya China na Afrika, Moshi alisema kuwa ushirikiano huo umekuwa na historia ndefu, na umeimarishwa siku hadi siku. Miaka mingi iliyopita, kwa kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la "Ukanda Mmojia na Njia Moja", China imeanzisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kijamii na bara la Afrika.
Moshi alisema: "Katika mambo ya biashara na uwekezaji, China imefuata njia ya kunufaishana, ambayo ni tofauti na ile ya nchi za magharibi. Biashara na uwekezaji kati ya Afrika na China inaendelea kukua kwa kasi kubwa mwaka hadi mwaka, yote hayo yamesukuma mbele uchumi wa Afrika kukua kwa kasi zaidi, na kuhimiza mambo ya kupunguza umaskini na kuongezeka kwa nafasi za ajira barani Afrika.”
Agosti 24, mkutano na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za BRICS umeamua kuzikaribisha nchi za Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa wanachama wapya, na uanachama utaanza kufanya kazi Januari 1, Mwaka 2024. Nchi nyingi zaidi za Afrika zimejiunga na familia ya BRICS, ushirikiano kati ya Afrika na China utaendelea kufikia kilele kipya, na nchi zenye masoko yanayojitokeza na nchi zinazoendelea pia zitafanya kazi muhimu zaidi katika usimamizi wa dunia nizma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma